KUHUSU RESET IMPACT
RESET IMPACT ni taasisi ya elimu ya afya na mtindo wa maisha inayolenga kuwasaidia wanaume kujenga afya bora, nidhamu binafsi na maisha yenye kusudi.
Tunaamini kuwa mwanaume mwenye afya njema, mwenye nidhamu na anaye jitambua ndiye msingi wa familia imara na jamii yenye maendeleo.
Kupitia elimu, programu za mafunzo, vitabu, ushauri na virutubisho vya afya, tunawapa wanaume maarifa na mifumo ya vitendo ya kuwasaidia kushinda changamoto zinazowazuia kufikia uwezo wao kamili.
Dhamira yetu ni kuleta mabadiliko chanya kwa mwanaume mmoja mmoja, ili kujenga familia bora na jamii yenye nguvu.
Dira (Vision)
Kuwa taasisi inayoongoza Afrika katika elimu ya afya,Mtindo wa maisha na maendeleo ya mwanaume.
Dhamira (Mission)
Kuwawezesha wanaume kuishi maisha yenye afya, nidhamu na kusudi kupitia elimu, na mifumo ya vitendo.
Maadili Yetu
Afya
Nidhamu
Kusudi
Uadilifu
Uwajibikaji
Mabadiliko Endelevu